wananchi wilayani Chamwino mkoani Dodoma wametakiwa kuwa mstari wa mbele kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii

DODOMA

Katika kuondokana na gharama kubwa za huduma ya matibabu,wananchi wilayani Chamwino mkoani Dodoma wametakiwa kuwa mstari wa mbele kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii ili kujihakikishia uhakika wa matibabu wakati wowote ikiwa ni utekelezaji wa vipaumbele vya  Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli katika sekta ya Afya

Sekta ya Afya ni moja ya sekta muhimu kwa maendeleo ya taifa ambapo Rais Dr Magufuli ameahidi kutatua kero za sekta ya Afya ambapo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma imeanza kusimamia vipaumbele hivyo kwa kuhimiza wananchi kujiuunga na mfuko wa Afya ya Jamii

Farida Mgomi ni mkuu wa wilaya ya Chamwino akizungumza na wananchi katika vijiji vya Manda,Mpwayungu,Mlowa anasema kuwa mfuko wa Afya ya jamii unafaida kubwa kwa wananchi katika kupata huduma za matibabu kwa uhakika

Comments

comments