Wananchi wilayani Arumeru wamemwandikia barua afisa mtendaji kumtaka kuondoka katika ofisi.

Arumeru

Wananchi wapatao 513 wa kijiji cha Imbaseni kata ya Maji ya chai  wilayani Arumeru wame mwandikia barua afisa mtendaji wa kijiji chao ya kumtaka kuondoka katika ofisi ya kijiji hicho kwa kukwamisha maendeleo ya ujenzi wa zahanati wakati wamesha changisha shilling milioni kumi za kuanzia ujenzi

Wakizungumza katika mkutano wa adhara uliongozwa na mwenyekiti wa kijiji cha Embaseni bwana Gadiel mwanda wananchi hao wamemtuhumu bi Glory Urio kukwamisha ujenzi wa zahanati kwa maslai yake binafsi bila kutoa sababu za msingi za kuzuiya ujenzi huo na kukataa kuuzuria kikao cha serikali ya kijiji .

Mwenyekiti wa kijiji hicho Gadiel Mwanda amesema mtendaji huyo amekua akikwamisha maendeleo ya kijiji chake kwa kuzuiya maendeleo ya ujenzi wa zahani pamoja na ujenzi wa barabara, shule za awali kwa wanachi wa kijiji chake kwa itikadi za kisiasa  .

Amesema mtendaji huyo analeta siasa katika maswala ya maendeleo kwakua kijiji katana jimbo zima la Arumeru linaongozwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema hivyo maendeleo hayo yanawapa kuonekana kutekeleza ahadi zao za kuwapa wananchi kupata mahitaji muhimu

Wakina mama wa kijiji hicho wamemtaka mwenyekiti huyo kusimamia ujenzi wa zahanati kwani wamekua wakipoteza ndugu na kina mama wengine kufia bara barani wakienda kujifungua kwa kutembea umbali mrefu kufuata uduma eneo la Tengeru iliyopo hospital ya wilaya .

Mtendaji huyo Glory Urio alipo tafutwa ofisini kwake kujibu tuhuma hizo zinazo mkabili alishindwa kuonyesha ushirikiano kwa vyombo vya habari kwa kutafutwa ofisini kwake akuepo na alipo pigiwa simu  alijibu simu ni mbovu na kuandika ujumbe mfupi wa maeneno kua wananchi hao wameshindwa kufuata taratibu na sheria za nchi za ujenzi wa zahanati na uwibuaji wa miradi.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments