Wananchi wa kijiji cha MKOYO, mkoani Dodoma kullamikia mradi wa maji.

mradi wa maji

Wananchi wa kijiji cha MKOYO, tarafa ya HOMBOLO manispaa ya DODOMA, wamelalamikia kutokamilika kwa mradi wa maji ulioanzishwa kijijini hapo miaka mitano iliyopita.

Wamesema kuwa mradi huo uliofadhiliwa na Benk ya Dunia kwa thamani ya MILIONI MIA SITA SITINI ulipaswa kukamilika miezi sita tangua kuanza kwa ujenzi wake lakini imepita miaka mitano bila kukamilika.

Wamesema mpaka sasa mradi huo ambao upo chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma unatoa huduma ya maji katika vituo vitatu tu kati ya vituo 24 vilivyotakiwa kujengwa na kutoa maji.

Mwenyekiti wa kijiji cha hicho ENLEY NGUBESI, ameiambia TBC kuwa, kutokamilika kwa Mradi huu umesababisha wananchi wake waendelee kutaabika kwa kunywa maji machafu kitu kinachoatarisha hali ya afya ya wanakijiji hao.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts