Wananchi mkoani Mtwara waombwa kujitokeza kwa uwingi katika mapokezi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.

Ndendego

Bi Halima Dendego

Wananchi mkoani Mtwara waombwa kujitokeza kwa uwingi katika mapokezi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli anayetarajia kufanya ziara yake ya kikazi mkoani humo hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake mkuu wa mkoa mtwara Bi Halima Dendego amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Mh raisi ikiwa ni mara yake ya kwanza kudhuru mkoani humo ikiwa ni pamoja na kuzindua shuguli mbalimbali za kiuchumi tangu achaguliwe kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Bi Halima amesema kuwa, miongoni mwa mambo Mh raisi ni kutembaea Kiwanda cha cement cha Dangote, Bandari ya Mtwara, Ofisi za NMB kanda ya kusini, Ofisi za benki kuu kanda ya kusini, pamoja na Eneo la Tanesco ambapo ujenzi wa mashine mpya ya kusambazaji umeme katika mikoa ya mtwara na lindi na kuhitimisha ziara yake katika viwanja vya mashujaa ambapo atapata wasaa wa kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa mheshimiwa John Pombe Magufuli kufanya ziara yake katika mikoa ya kusini mwa Tanzania inayoelenga kuleta tija ya maendeleo katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Imeandaliwa na Stanley Burushi

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments