Wananchi mbalimbali wameishauri serikali kuunda tume maalumu itakayowasaidia vijana wengi waliomaliza vyuo vikuu na wasio na ajira kujiepusha kufanya matukio ya uvunjifu wa amani.

Sibuka Sauti ya Jamii

Wananchi mbalimbali wameishauri serikali kuunda tume maalumu itakayowasaidia vijana wengi waliomaliza vyuo vikuu na wasio na ajira kujiepusha kufanya matukio ya uvunjifu wa amani.

Wakizungumza na SIBUKA FM, BW. GANGANAH MWERI amesema vijana wengi ni waoga katika kuanza maisha hivyo kama uwezekano upo serikali inatakiwa kuhakikisha wanawapa mikakati mizuri wanapokuwa vyuoni.

Naye BW. JAMES KIMELA amewashauri vijana kujikita katika kazi mbalimbali hata za kujitolea ili kupata ujuzi wa kuwawezesha kupata uwezo wa kufanya kazi zao binafsi.

Aidha wamewaomba wazazi kuwafundisha watoto wao namna ya kukabiliana na maisha wanapomaliza masomo yao na kuwapa mitaji ya kuanza biashara kwa wazazi wenye uwezo.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments