Wanajeshi wa US wasambaza picha za utupu za wenzao wa kike

Wanajeshi wanawake wa Marine
Wanajeshi wanawake wa Marine

Wanajeshi wa Marekani kutoka vitengo tofauti vya jeshi wamekuwa wakionyeshana picha za uchi za wanajeshi wenzao wa kike kwenye mitandao.

Ripoti ya wiki iliyopita ilibaini picha nyingi za uchi zilizokuwa zikisambazwa na kitengo cha wanajeshi wanamaji wa zamani na wanahudumu kwa sasa katika mtandao wa Facebook kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Lakini BBC imeona picha ambazo wanajeshi wengine kutoka vitengo vyengine ambao wamesambaza mamia ya picha hizo.

Makao makuu ya kijeshi ya Marekani, The Pentagon, yamesema tabia hiyo ‘haiambatani’ na mila zake.

Wanajeshi wanaume wamekuwa wakitumia mtandao wa picha na video wa Anon -IB kuweka picha hizo za uchi za wanajeshi wenzao wa kike.

Wanajeshi hao kwanza huweka picha za wanawake hao wakiwa na nguo ambazo huzitoa katika kurasa za mitandao yao ya kijamii, na kuuliza wengine katika kundi hilo iwapo mmoja wao anapicha za uchi za mwanajeshi huyo, ambao huita ‘ushindi’ na wengine hutuma picha hizo za uchi.

#SIBUKAMEDIA

#BBC SWAHILI

Comments

comments

Random Posts