Wanaharakati waandamana kushutumu mauaji ya meneja wa tume ya uchaguzi Kenya.

Watetezi wa haki za kibinadamu wameandamana katika uwanja wa Uhuru Park, kushutumu kuuawa kwa afisa mmoja mkuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya Christopher Msando.

Bw Msando alitoweka Ijumaa na mwili wake ukapatikana ukiwa umetumwa viungani mwa jiji la Nairobi Jumamosi asubuhi.

Mwili wake ulitambuliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City Jumatatu.

George Kegoro kutoka shirika lisilo la kiserikali la Tume ya Haki za Kibinadamu Kenya (KHRC) amesema wana wasiwasi sana kwamba mauaji ya Bw Msando yatazua mtafaruku uchaguzi mkuu unapokaribia.

  • #SIBUKAMEDIA
  • #BBC SWAHILI

Comments

comments