Wamachinga wazuiliwa kufanya biashara zao barabarani.

maxresdefaultMkuu wa mkowa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wametakiwa kutofanya biashara zao kandokando ya barabara na sehemu zisizo sahihi ili kuepuka usumbufu kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar-es-Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam Paul Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema hataki kuona biashara hizo zikifanyika katika maeneo hayo kwani kwa kufanya hivyo kunaleta usumbufu mkubwa.

Makonda ameongeza kuwa inasikitisha kuona wafanyabiashara hao wakifanyia shughuli zao kando ya barabara kitendo ambacho kinapelekea usumbufu kwa madereva pamoja na wananchi wanaotumia barabara hizo na wakati mwingine kupelekea wizi kutokana na msongamano.

Katika hatua nyingine Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Dar-Es-Salaam kuhakikisha wanawatafutia maeneo ya kufanyia biashara zoezi ambalo linapaswa kufanyika ndani ya siku 14.

Comments

comments