Walionusurika vyeti feki, wajiandaa wimbi la pili linakuja.

2

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hasani Suluhu amewatumia salamu watumishi ambao walinusurika katika zoezi la ukaguzi wa watumishi hewa, vyetu feki na mishahara hewa akisema wajiandae kwani wimbi la pili linakuja kwao.

 Makamu wa Rais amesema hayo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu kitaifa yaliyofanyika mjini hapa.

 Amesema kuwa wapo ambao katika awamu ya kwanza ya uhakiki wa vyetu hawakupitiwa na wengine walijificha lakini katika awamu ya pili zoezi hilo litampitia kila mtumishi ambaye alinusurika awali.

 Amesema kuwa serikali inahitaji watumishi wanaotimiza wajibu wao kwa wakati hivyo kama kuna mtu mzembe kazini viongozi wasisite kumuondo kwani hakutatokea pigo la ajira nchini.

Aidha amesema kuwa serikali imeanza kujenga mifumo ya kuweka ‘kazi data’ za watumishi wa umma pamoja na kuweka mfumo wa kutoonana katika kutoa huduma.

 Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika amesema kuwa huwezi kuwa mzalendo kama si mwadilifu na huwezi kuwa mwadilifu kwama si mzalendo hivyo kuwataka watanzania kuhakikisha wanakuwa wazalendo na waadilifu.

 Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Andy Karas amesema kuwa wao kama mashirika ya maendelao wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika mapambano ya vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

 Kaulimbiu katika maadhimisho hao ni wajibika:piga vita rushwa, zingatia maadili, haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumu wa kati.

 #SIBUKAMEDIA

Comments

comments