Wakulima wialaya ya kasulu waimeomba idara ya kilimo wilayani humo kuwapatia pembjeo za kilimo.

mahindi+2

Wakulima katika halmashauri ya wialaya ya kasulu mkaoni kigoma waimeomba idara ya kilimo wilayani humo kuwapatia pembjeo za kilimo pamoja na mbegu zitakazo wasaidia kuengoza uzalishaji wa mazao mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Wakizungumza na sibuka fm baadhi ya wakulima wa mazao ya biashara wilayani kasulu ikiwemo mihogo,maharage pamoja na mahindi wamesema ili kukakbilina na kilimo bora sambamba na upatikanaji wa mazao mengi katika msimu wa mavuno inabidi idara ya kilimo wilayani humo kuangalia namna nzuri ya kuwawezesha upatikaji wa pembejeo zinazoendana na kilimo cha kisasa kwa wakulima wilayani humo.

hogo

Aidha kwa upande wake Afisa kilimo wa wilaya ya kasulu  bw. John Philimoni ameiambia sibuka fm kuwa  serikali ina anaangalia kwa makini suala la uapatikanaji wa pembejeo kwa wakulima huku akibainisha kuwa kilimo cha kutumia pembejeo kimekuwa na faida kwa wakulima kutokana na upatikanaji wa mavuno ya kutosha ukilinginisha na kilimo cha kawaida.

Hata hivyo ameongeza kuwa kabla ya kuanza kwa kilimo cha pembejeo mkulima alikuwa na uwezo wa kupata gunia 3 mpka 4 za maharage kwa heka moja, wakati kwa sasa hali imekuwa ni nzuri zaidi kwani mkulima anao uwezo wa kupata gunia 6 mpka 8 za kwa heka moja kutokana na kilimo cha pembejeo.

  • Mwandishi : Saulo Steven
  • #SIBUKAMEDIA.

 

Comments

comments