Wakenya wanaofika Tanga waongezeka uchaguzi ukikaribia.

kenyaaaaa

Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Kenya kufanyika, Tanzania imeshuhudia wimbi kubwa la wageni kutoka nchini Kenya hasa katika miji ambayo iko karibu na mpakani kama vile Tanga, Arusha na kuendelea.

Wandishi wetu Aboubakar Famau ambaye alikuwa mjini Tanga, alikutana na baadhi ya wageni hao ambao baadhi walidai wameingia Tanzania kwa ajili ya matembezi huku wengine wakikiri kwamba wafika nchini humo wakihofia huenda baada ya uchaguzi kukatokea machafuko kama ilivyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

“Mimi sijakimbia uchaguzi. Nimekuja kwa ajili ya matembezi kwa sababu ndio nimepata fursa wakati huu,” alisema Sumeiyan Sharif akiwa safarini kutoka Mombasa kuelekea jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Sumeiya aliongeza kusema kuwa, ni kweli watu wingi wamesafiri kama moja wapo ya tahadhari kwa kuhofia lolote linaweza kutokea.

Licha ya mji wa Tanga kuwa karibu na mpaka wa Kenya, mara nyingi mji huo unakuwa hauna pilka pilka za kibiashara kama ilivyo katika mikoa mingine ya Tanzania.

#BBC

Comments

comments

Random Posts