Wakenya na Wasomali 72 Watimuliwa Marekani.

IMG_20170512_152839_451

Serikali ya Marekani imewatimua watu 72 kutoka Kenya na Somalia kutokana na matatizo mbalimbali ya uhamiaji.

Waliofurushwa ni Wakenya watano na hao wengine wana asili ya Kisomali, gazeti la Star limeripoti.

Afisa mmoja wa serikali ameambia BBC kwamba ni kweli watu hao wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi lakini akasema serikali ya Kenya bado inatafuta taarifa zaidi kuhusu utambulisho wao.

Waliwasili uwanja wa ndege mapema Ijumaa.

Mwezi Januari, Wakenya wawili na Wasomali 90 waliwasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta baada ya kufukuzwa Marekani kutokana na matatizo mbalimbali ya uhamiaji.

Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi kukabiliana na wahamiaji haramu walio nchini Marekani tangu aingie madarakani mwezi January.

#BBC SWAHILI

#SIBUKA MEDIA

Comments

comments