Wakazi wa Manispaa ya ILALA, Kutumia hospital mpya ya Chamanzi.

Wakazi wa Manispaa ya ILALA jijini DAR-ES-SALAAM wametakiwa kuitumia hospitali mpya ya CHAMAZI itakayofunguliwa hivi karibuni kwa usahihi katika kupata huduma ya afya bora.

Mkuu wa wilaya ya ILALA BI. SOPHIA MJEMA ametoa wito huo leo wakati akikagua hospitali hiyo na kuongeza kuwa amefurahishwa na ujenzi wa hospitali hiyo unaofadhiliwa na serikali ya KOREA,na kwamba kukamilika kwa hospitali hiyo kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya afya hasa kwa kina mama.

BI.MJEMA amesema kuwa katika manispaa ya ILALA wananchi wengi wamekuwa wakikimbilia kutibiwa katika hospitali ya amani jambo linalopelekea hospitali hiyo kuzidiwa hivyo kukamilika kwa hospitali hiyo kutatatua changamoto ya wagonjwa wanaokimbilia hospitali ya amani.

Mwandishi: Stanley Burushi

#SIBUKAMEDIA

Hospitali hiyo mpaka kukamilika kwake itagharimu jumla ya dola milioni themanini na nane na milioni mia nane.

Comments

comments