Wakazi mkoani Kigoma wamelalamikia shirika la umeme Tanzania tanesco.

tanesco

Wakazi mkoani kigoma wamelalamikia shirika la umeme Tanzania tanesco mkoani humo kwa kuwaingiza katika mfumo wa matumizi makubwa ya umeme wa luku pasipo wao kufahamu kinachoendelea juu ya matumizi hayo.

Wakizungumza na sibuka fm baadhi ya wakazi katika maeneo tofauti ya mkoa wa kigoma wamesema kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya umeme wa luku wamekuwa wakilipa pesa ambazo haziendani na kiwango cha umeme wanachopatiwa  na hivyo kulitaka shirika hilo kuandaa mkakati maalumu wa kuwafundisha wanachi juu ya matumizi makubwa na madogo pindi wanapo nunua umeme wa luku.

Aidha kwa kuapande wake afisa uhusiano huduma na  kwa wateja tanesco mkoani humoa bw.Emmanuel Batuba ameiambia sibuka fm kuwa wamekuwa wakipata malalamiko  hayo kutoka kwa wateja na kubainisha kuwa matumizi makubwa kwa watejea wa luku hutokaan na wateja wenyewe kununua umeme kidogokidogo na hivyo kujikuta katika matumizi makubwa.

Hata hivyo bw. ametuba ameshauri wateja na jamii kwa ujumla koani humo kununua umeme usiopungua wala kuzidi shilingi elfu tisa kila mwezi na ili kusaidia kuepukana na matumizi hayo na kuwa katika matumizi ya kawaida.

  • Mwandishi : Saulo Steven
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments