Waghana wapiga kura kumchagua Rais

Wananchi wa  Ghana wanaendelea na zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kumchagua Rais pamoja na wabunge licha ya  mashaka yaliyojitokeza juu ya uwezo wa tume ya uchaguzi nchini humo.36673349_303

Zoezi hilo la uchaguzi linaendelea mnamo wakati majina kadhaa  ya watu waliojiandikisha kupiga kura yakikosekana katika daftari la wapiga kura.

Licha ya mapungufu hayo maafisa wa serikali  nchini humo wametoa mwito kwa wananchi kuendelea kuwa na imani na tume ya uchaguzi nchini humo na kudumisha amani.

Ushindani mkubwa katika uchaguzi huo uko katika kinyanganyiro cha nafasi ya Rais ambapo Rais wa sasa  John Draman Mahama anachuana vikali na kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini humo Nana  Akufo-Addow. Hii ni mara ya tatu mgombea huyo wa upinzani Akufo Ado kuwania nafasi hiyo baada ya kufanya hivyo katika uchaguzi wa mwaka 2008 na 2012.

Kumekuwa na kura chache za maoni  kuhusiana na uchaguzi huo lakini wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa  wanasema kura za nafasi ya urais zinaweza zikakaribiana kutokana na ushindani utakaonyeshwa na mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini humo.

#DW IDHAA YA KISWAHILI

Comments

comments