wafanyakazi wa Kampuni ya EAST AFRICAN wamemaliza mgomo walioundesha kwa siku mbili baada ya uongozi kukutana na Katibu Tawala wa wilaya ya KINONDONI.

Hatimae wafanyakazi wa Kampuni ya EAST AFRICAN wamemaliza mgomo walioundesha kwa siku mbili baada ya uongozi kukutana na Katibu Tawala wa wilaya ya KINONDONI BI.GIFT MSUYA  na kukubali kufanya mabadiliko.

Hatua hiyo imefikiwa jijini DAR ES SALAAM baada ya wafanyakazi hao kugoma kuendelea na kazi.

BI.GIFT ameuagiza uongozi wa Kampuni hiyo kuhakikisha wanalipa mishahara ya wafanyakazi,kuwapa mikataba ya kisheria  wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika Kampuni hiyo.

Kwa upande wake Mhandisi  wa Kampuni hiyo BW. GABRIEL MAKONDI amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuahidi kutekeleza yote waliyokubaliana na uongozi wa manispaa ya KINONDONI hadi kufikia mwishoni mwa mwezi septemba 2017.

Mmoja wa wafanyakazi hao BW.HAJI ADAMU ameushukuru uongozi wa manispaa ya KINONDONI kwa kuingilia Kati mgogoro huo, kwa kuwa tatizo hilo limewasumbua kwa muda mrefu.

Wafanya kazi wa kampuni ya EAST AFRICAN COMPANY (S.E.C) waligoma kwa siku mbili kushinikiza Kampuni hiyo kuwalipa mishaara na kutopewa mikataba ya kazi  kwa kuwa hawakuwahi kupewa mikataba tokea Kampuni hiyo ianzishwe.

  • Mwandishi : Edwin Odemba na Tuse Kasambala.
  • Mhariri : Amina Chekanae.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments