Wafanyabiashara watishia kubomoa vibanda

WA F A N Y A  B I A S H A RA wilayani Sikonge mkoani Tabora wametishia kubomoa vibanda vyao na kuchukua matofali na bati zao kufuatia uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kutaka kuchukua vibanda hivyo.
Wakizungumza kwenye kikao kati ya wafanyabiashara, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri walisema kitendo hicho wanakipinga kwani haki yao inapokwa.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa wilaya hiyo Peter Nzalalila alisema vibanda hivyo walivijenga kwa gharama zao baada ya uongozi wa halmashauri kugawa maeneo ya ujenzi mwaka 2003 na walikuwa wakipewa risiti tu na kulipia. Waliongeza kuwa kipindi hicho hawakupewa mikataba inayoonesha mara baada ya miaka fulani watavirejesha kuwa mali ya halmashauri.

Aidha walishangazwa kuandikiwa barua na tangazo kwenye gazeti kuwa vibanda hivyo sasa vitakuwa mali ya halmashauri na wao watalazimika kulipia ushuru halmashauri. Nzalalila alisema wengi wao wakiwemo wafanyabiashara wanalipia ushuru kwa wamiliki waliojenga hivyo ikiwa halmashauri inataka ushuru ilitakiwa kukaa na wamiliki sio wao.

Kwa mujibu wa Nzalalila, halmashauri tayari ilishakosea katika kutengeneza vyanzo vya mapato sasa kwa sababu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kabana kila halmashauri nchini kukusanya mapato kwa asilimia 80 inakuwa tabu kwao.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Hanifa Selengu aliwasihi wafanyabiashara hao kukaa na halmashauri kutatua mgogoro huo na kwamba serikali na wafanyabiashara ni ndugu.

Comments

comments

Random Posts