Wafanyabiashara ndogo ndogo mjini DODOMA wameishukuru serikali.

Wafanyabiashara ndogo ndogo mjini DODOMA wameishukuru serikali kwa kuwapa nafasi ya kufanya biashara zao bila kubughudhiwa .

Akizungumza na SIBUKA FM kiongozi wa wafanyabiashara hao SEIFU OTHUMANI amesema siku za nyuma walikuwa wakikutana na changamoto mbalimbali zilizochangia kudidimiza maendeleo yao.

OTHMAN ametaja  adha walizokuwa wakizipata kuwa ni pamoja na kufukuzwa katika maeneo ya biashara, kunyang’anywa mali zao na kulazimishwa kupa faini kubwa kuliko kiwango halisi.

Wafanyabiashara hao wamempongeza Rais JOHN MAGUFULI  kwa kuwatetea wafanya biashara wadogo na hivyo kuwawezesha kujiajiri na kuendesha maisha yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma GODWIN KUNAMBI amesema Manispaa yake iko kwenye mpango wa kuandaa eneo la MAKOLE kuwa eneo maalum la wafanyabiashara hao wadogo wadogo.

  • Mwandishi : Barnaba Kisengi.
  • Mhariri : Amina Chekanae.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments