Wafanya Biashara wa Ilala watakiwa kutopandsha bei za vyakula kuelekea msimu huu wa mfungo.

buguruni

Wafanyabiashara wa masoko katika manispaa ya ILALA jijini DAR ES SALAAM wametakiwa kutopandisha bei za vyakula kuelekea msimu huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya ILALA,SOPHIA SIMBA wakati alipofanya ziara ya kushutukiza katika masoko ya BUGURUNI na ILALA kujionea hali halisi ya miundombinu na kuongeza kuwa kumekuwepo na hali ya kupanda kwa vyakula .

Amesema bei vya vyakula hasa nafaka katika masoko sio mbaya sana hivyo wafanyabiashara wajitahidi kutopandisha bei mwezi mtukufu  wa ramadhani.

Mwenyekiti wa soko la BUGURUNI,BW.SAID MASOUD amemweleza mkuu wa wilaya huyo kuwa changamoto kubwa inayowakabili wafanyabiashara hao ni ubovu wa miundombinu hasa vyoo kujaa maji wakati wa mvua.

Awali Mkurugenzi wa manispaa hiyo BW.MSONGELA PALELA amesema manispaa ina mpango wa kuboresha masoko yote yaliyopo ndani ya manispaa hiyo kwa kujenga majengo ya ghorofa ili kila mfanyabiashara apate nafasi ya kupanga bidhaa.

  • ¬†Mwandishi : Stanley Burushi
  • Mwariri : Amina Chekanae
  • #SIBUKAMEDIA

 

 

Comments

comments