Waandishi wa habari,wadau wamejitokeza kuaga mwili wa MAYAGE STEPHEN MAYAGE.

Mayage

Waandishi wa habari,wadau wa habari,ndugu jamaa na marafiki wamejitokeza kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari mkongwe marehemu MAYAGE STEPHEN MAYAGE.

Katika ibada maalum iliyofanyika nyumbani kwake MBWENI jijini DAR ES SALAAM viongozi mbalimbali wa wamejitokeza akiwemo mbunge wa MTAMA NAPE NNAUYE,na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,HUMPHREY POLEPOLE.

Akizungumza wakati wa iada hiyo NAPE amesema amesikitishwa na kifo hicho na kusisitiza waandishi wa habari kumuenzi kwa kufuata mema aliyokuwa akifanya .

Aidha NAPE amekiri kuwa CCM kimepata pigo kwa kifo cha marehemu MAYAGE STEPHEN MAYAGE  kwa kuwa marehemu alikuwa ni mwanachama wa kweli ndani ya CCM.

Marehemu MAYAGE STEPHEN MAYAGE alifariki dunia siku ya jumatatu wakati akipatiwa matibabu ya kifua kikuu katika hospitali ya misheni ya MBWENI  na amezikwa leo jijini DAR ES SALAAM.

Bwana alitoa nae ametwaa jina lake lihimidiwe AMEN.

  • #Sibukamedia

Comments

comments