Viongozi wametakiwa kuelimisha suala la maadili na kuhakikisha wanaishi na kuzingatia kanuni za maadili kwa wao kuwa mfano.

Viongozi mbalimbali na wasimamizi wa kazi wametakiwa kuelimisha suala la maadili na kuhakikisha wanaishi na kuzingatia kanuni za maadili kwa wao kuwa mfano.

Kaimu Mkurugenzi wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais BW.LAMBERT CHIALO ametoa agizo hilo jijini DAR ES SALAAM na kusisitiza kuwa watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa kufuata taratibu zilizowekwa na ofisi.

Amesema moja ya changamoto kubwa katika ofisi nyingi ni utoro kazini,matumizi mabaya ya taarifa  za serikali pamoja na watumishi wengi kuvaa mavazi yasiyofaa kazini ikiwemo flana,nguo zinazoonyesha sehemu za mwili,nguo zinazobana pamoja na mavazi mengine yasiyofaa.

Kwa mujibu wa taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma watumishi wa Umma 2755 walichukuliwa hatua za kinidhamu ambapo watumishi 1142 walifukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ambapo utoro ilikuwa asilimia 54,ubadhirifu wa mali za Umma asilimia 20 na uvaaji wa nguo zisizofaa asilimia 26.

BW. CHIALO amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa kuzingatia sharia,kanuni na taratibu zilizopo na kuwasisitiza waache kufanya kazi kwa mazoea na kutimiza wajibu wao.

#SIBUkAMEDIA

Comments

comments