Viongozi wa kidini wa Afrika kujadili njia ya kuzuia uchochezi

Viongozi wa kidini kutoka nchi mbalimbali za Afrika watakutana wiki ijayo mjini Addis Ababa kujadili njia ya kuzuia uchochezi ambao utasababisha uhalifu wa kikatili.

Taarifa iliyotolewa na kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa inasema, viongozi hao kutoka dini mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria mkutano utakaofanyika tarehe 9 hadi tarehe 11 Mei, na kuendeleza mkakati wa kuzuia na kupambana na uchochezi wa unyanyapaa, uhasama na matumizi ya nguvu barani Afrika.

Comments

comments