Vikwazo dhidi ya Iran: Marekani haiwezi kutuzuia kuuza mafuta, asema waziri

Alisema kuwa mkataba huo ulifeli kuafikia malengo yake muhimu ya kuzuia Iran kutengeneza bomu la kinyuklia na hayakuangazia vitendo vya ukandamizaji vya Iran mbali na utengenezaji wa silaha za masafa marefu na kuunga mkono ugaidi.

Rais wa Iran Hassan Rouhani ambaye anasisitiza kuwa mpango wake wa kinyuklia ni wa amani, amemshutumu rais Trump kwa kuanzisha vita vya kisaikolojia na kukataa mazungumzo ya ana kwa ana na yeye iwapo vikwazo hivyo vitaendelea.

Siku ya Jumanne , Marekani ilirudisha vikwazo dhidi ya Iran ikilipiga marufuku taifa hilo katika ununuzi wa noti zake za dola, biashara ya Iran ya dhahabu na madini mengine pamoja na sekta ya magari.

Mnamo mwezi Novemba awamu ya pili ya vikwazo vikali zaidi vitawekwa dhidi ya waendesha bandari ya Iran, sekta ya kawi, uchukuzi wa majini pamoja na sekta ya uundaji wa meli.

Vikwazo dhidi ya kuuza mafuta na maswala ya ubadilishanaji wa fedha kati ya taasisi za kifedha za kigeni na benki kuu ya Iran pia zitaathiriwa.

Katika Ujumbe wa twitter , bwana Trump alionya, ”mtu yeyote anayefanya biashara na Iran hataruhusiwa kufanya biashara na Marekani . Nataka amani duniani sitaki sina mengi”.

Baadye bwana Zarrif alijibu katika mtandao wa twitter akisema: Kujionyesha na jumbe nyingi za Twitter zenye maneneo yenye herufi kubwa hakutabadilisha ukweli kwamba dunia imechoshwa na ukoloni wa Marekani..”

“Kusitisha biashara na Marekani na kuharbu kazi 100,000 hakututii wasiwasi, lakini ulimwengu hautafuata madikteta wanaotumia twitter. Uliza EU, Urusi, China na washirika wetu wengi wa kibishara”.

 

Comments

comments