Vijiji tisa(9) mkoani Kigoma vimekumbwa na tatizo ukosefu wa maji.

KIGOMA

Jumla ya vijiji tisa vilivyopo katika halmashauri ya wilaya ya KIGOMA vimekumbwa na tatizo la ukosefu wa maji kufuatia kuharibika kwa mradi maji uliopo katika kijiji cha mkongoro one {01}kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Wakizungumza na sibuka baadhi ya wakazi kutoka katika vijiji hivyo wamesema, baada ya kuharibika kwa chanzo hicho, inawalazimu kutembea umbali mrefu ili kuweza kupata huduma ya maji ambayo nimuhimu kwa maisha ya binadamu.

Kwaupande wake diwani wa kata ya MKONGOLO ambayo ni miongoni mwa kata zilizoathirika na kuharibika kwa chanzo hicho BW. MORANI HUSSEN ameeleza kuwa, kutokana na uharibifu huo jamii imekumbwa na  adha ya kokosa maji ambayo wangeyatumia katika matumizi mbalimbali  sambamba na kutoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini juu ya maji wanayoyatumia kwa sasa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kutokea.

Aidha kwa upande wake , mhandisi wa Halmashauri ya KIGOMA BW, LEO-LESPESIUS ameiambia sibuka fm kuwa  tayari serikali imeshabaini adha wanayoipata wakazi wa vijiji hivyo kwa sasa, na kusema kuwa tayari wameanza taratibu za  kurekebisha  mradi huo ili huduma ya maji iweze kurejea haraka iwezekanavyo  katika vijiji hivyo.one {01},

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts