Vijana, Wamewaasa kubadili fikra ya kuajiriwa na badala yake kujiajiri.

vlcsnap-2017-03-24-09h58m31s999

Naibu wazir wa kazi,ajira na vijana,Bw.Anton Mavunde amewaasa vijana kubadili fikra ya kuajiriwa na badala yake kujiajiri.

Amesema hayo mapema leo katika kongamano la kitaifa na kimataifa lenye kushirikisha zaidi ya vijana 1200  linalofanyika  Ostabey jijini Dar esalaam kuwa vijana wengi wamekuwa wakizunguka na vyeti na kujikuta wakipoteza muda mwingi kufanya mambo yasiyo na msingi yanayosababishwa na kukata tamaa.

Naibu waziri Mavunde amewashauri vijana kuacha kukaa vijiweni kwa kukata tamaa na badala yake wafanye kazi kwakuwa hekima,busara,nidhamu ndo msingi wa mafanikio.

Nae mwenyekiti wa Taswe Bi.Anna Matinde amesema kuwa mkutano huo wa kubadili fikra na kuwajengea uwezo ili waweze vijana kujiajiri utakuwa ukifanyika mara nne kwa mwaka.

Kongamano hilo limeandaliwa na chama cha  wajasiriamali wanawake  cha kuweka na kukopa cha Tanzania saccos (Taswe) wakishirikiana na Remnant singers kwa pamoja wameandaa kongamano litakalofuatia na maonyesho yanayoshirikisha wajasiriamali kutoka nchini Comoro,kenya,Rwanda na Dubai.

Mwandishi: Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments