vijana kujiajiri kupitia ubunifu kampuni ya simu ya mkononi ya tigo

DAR ES SALAAM

Katika kukuza teknolojia ya mawasiliano na kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia ubunifu kampuni ya simu ya mkononi ya tigo imetoa udhani wa masomo unaogharimu shilingi milioni mia tatu na kumi kwa wanafunzi tisa wa vyuo vikuu wanaosoma masuala ya TEHAMA.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar Es Salaam mkurugenzi mkuu wa tigo bwana DIEGO GUTIERREZ amesema kuwa udhamini huo unalenga kuwasaidia vijana wabunifu kutumia uwezo wao kurahisisha shughuli za kijamii zinazotegemea  teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA na vijana hao kujiajiri na kupunguza wimbi na vijana wasio na ajira nchini.

Comments

comments

Random Posts