Vifo vya kinamama vinavosababishwa na uzazi wakati wa kujifungua vimeonekana kuwa vingi kutokana na mazingira,miundombinu na ukosefu wa kifedha.

AGE

Vifo vya kinamama vinavosababishwa na uzazi wakati wa kujifungua vimeonekana kuwa vingi kutokana na mazingira,miundombinu  na ukosefu wa  kifedha unaopelekea wengi wao kupoteza maisha

Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa TAWLA Bi. Tike Mwambipili wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Umoja wa wanawake wanasheria  Tanzania kwa viongozi amesema kuwa kutokana na ugumu wa maisha na dharura zinazojitokeza kama kuharibika kwa mimba kusikotarajiwa hupelekea wanawake wengi kupoteza maisha na kutaka suala zima la bajeti katika afya ya uzazi kuongezwa.

Ameongeza kuwa wanawake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kuanzia utotoni ambapo muda mwingi wamekuwa wakikabiliana na vikwazo kama kudhalilishwa,kubakwa na kuonewa na hata kujikuta wakipata  mimba za utotoni jambo ambalo hukwamisha ndoto na malengo yao ya baadae.

AGA

Amebainisha kuwa sera ya bajeti ya uzazi nchini ikiainishwa kwa mchanganuo itasaidia kupatikana kwa fedha  na zaidi ambazo zitalenga kupunguza vifo kwa kinamama pamoja na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike. 

Imeandaliwa na Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments