Upinzani ”wapata ushindi wa mapema” Gambia

bbbbb

Matokeo ya kwanza kutoka uchaguzi wa urais nchini Gambia yanampa mgombea wa upanzani Adama Barrow ushindi dhidi ya Rais Yahya Jammeh.

Mwandishi wa BBC nchini Gambia anasema amepata thibitisho kuwa bwana Barrow ameshinda kwenye mji mku Banjul.

Hata hivyo ni chini ya asilimia 15 ya karibu wapiga kura 890,000 waliosajiliwa ndio imehesabiwa.

Wanajeshi na polisi hii leo wameweka vituo vya ukaguzi kwenye barabara zinazoingia na kutoka mji mkuu.

Serika ilizima huduma za mitandao na kufunga simu za kimataifa wakati uchaguzi ulikuwa ukiendelea.

Bwana Jammeh ameitawala Gambia tangu mwaka 1994 kufuatia mapinduzi ya kijeshi na sasa anawania muhula wa tano.

#BBC

Comments

comments