Ulinzi na usalama za Wilaya ya Kondoa na Chemba Kuhimarishwa

FM

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa Dr,Binilith Mahenge ameziagiza kamati za ulinzi na usalama za Wilaya ya Kondoa na Chemba kuhakikisha wanaimarisha Ulinzi katika maeneo yao ili kuepukana na vitendo vya kigaidi ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika baadhi ya maeneo hapa nchini

Dr.Mahenge ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake katika wilaya hizo ambapo akiwa wilayani Kondoa aliitaka kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kuhakikisha wanawahimiza watendaji wa kata na vijiji kuwa na vikao vya kuwatambua wageni wote wanaoingia katika wilaya hiyo

Na hii leo akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya chemba Mahenge amesema kutokana na kukua kwa teknolojia suala la uhalifu nalo limekua likikua kwa kasi hivyo ni lazima kujiandaa kuyadhibiti matukio hayo kabla hayajajitokeza

Aidha Dr Mahenge amesisitiza kuwa ni lazima kuimarisha ulinzi nyakati zote na si mchana pekee kwani wahalifu wengi hufanya shughuli zao wakati wa usiku ambapo pia kamati za ulinzi na usalama za kata na vijiji ni lazima zifikiwe na kuelekezwa mambo ya kujadili katika kukabiliana na vitendo hivyo

Awali akiwasilisha taarifa ya Wilaya yake Mkuu wa Wilaya hiyo Mh.Simon Odunga amesema hali ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo ni mzuri japo kumekuwa na changamoto ya migogoro ya kimipaka kutokana na wilaya hiyo kuznungukwa na baadhi ya wilaya ambayo hata hiyo wamekwishaanza kuitatua

Mkuu wa Mkoa bado anaendelea na ziara yake katika wilaya na maeneo mbalimbali katika mkoa wake yenye lengo la kujitambulisha.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments