Uchunguzi umefanyika kwa mtoto anayeishi kwa kula mafuta ya kula, sukari, pamoja na maziwa.

IMG-20170523-WA0013

Uchunguzi uliofanywa na madaktari kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili umebaini kuwa mtoto  SHUKURU KIPANGO  anayekula mafuta ya kula na sukari umebaini kuwa mtoto huyo ana upungufu wa madini ya chuma yaliyosababisha ugonjwa wa selinundu.

IMG-20170523-WA0014

Akizungumza jijini Dar es salaam daktari bingwa wa magonjwa ya damu na mkuu wa kitengo cha magonjwa ya damu  katika hospitali ya taifa Muhimbili DR. STELLAH RWEZAURA amesema kuwa ugonjwa wa selimundu ni wa kurithi  ambao ameurithi kutoka kwa wazazi wote wawili.

IMG-20170523-WA0008

RWEZAURA amebainisha kuwa tatizo hilo husababisha chembechembe nyekundu badala ya kuwa za mviringo anapokuwa na upungufu wa oksijen au anapopata maambukizi yoyote zinabadilika na kuwa katika umbo la ziro na zinapokuwa katika umbo hilo mwili unaziharibu na kutengeneza chembechembe nyekundu.

Aidha amesema kuwa tatizo la kuvimba kichwa na maumivu makali linatokana na  chembechembe nyekundu  zinapobadilika na kuwa katika umbo la  selimundu  haziwezi kupita katika mishipa midogo ya damu na kusababisha damu kushindwa kutembea kwenda upande wa pili na kuleta uvimbe mwilini.

IMG-20170523-WA0007

Nae BI. MWANABIBI MTENJE ambaye ni mama wa mtoto SHUKURU amewashukuru madakatari wa hospitali ya Muhimbili,serikali na wizara ya afya kwa msaada wao kwa kuwa mtoto huyo alikuwa akiteseka kwa muda mrefu.

  • Mwandishi :Tuse Kasambala
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments