Uchaguzi wa madiwani kutorudiwa.

tumeeeee

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, RAMADHANI KAILIMA amesema licha ya vyombo vya habari kuripoti matukio mbalimbali yaliyojiri katika uchaguzi mdogo wa madiwani,uchaguzi huo hautorudiwa.

BW.KAILIMA amesema hayo leo wakati akizungumza katika kipindi cha mahojiano maalum na watangazaji wa radio jijini DAR ES SALAAM.

Amesema kwa misingi na sheria za tume ya uchaguzi,uchaguzi umeenda vizuri kwa asilimia 95 na kusisitiza kuwa suala la watu kupigwa,mawakala kufukuzwa haliko mikononi mwa tume kwa hiyo hawezi kulisemea.

Akizungumzia sakata la kususia uchaguzi mkoani ARUSHA,KAILIMA  kwa madai ya wapinzani kufukuzwa kwa kutotimiza vigezo na masharti amesema kwa mujibu wa taratibu na sheria za tume kiongozi wa upinzani hakupaswa kufikia hatua hiyo kwa kuwa zoezi la kupiga kura lilianza asubuhi na yeye alisimamisha zoezi hilo kwa wafuasi wake saa tisa mchana.

Kuhusu suala la kukamatwa kwa meya wa UBUNGO,BONIFACE JACOB,BW.KAILIMA amesema tume hawana cheo cha wakala mkuu hivyo kujipachika cheo hicho ni kuvunja sheria na kwamba tume haiwezi kulisemea suala la kukamatwa kwake.

Jana kata 43 katika mikoa 16 nchini zilifanya uchaguzi mdogo wa madiwani ambapo matokeo ya awali yanaonyesha upinzani mkali baina ya CCM na CHADEMA.

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments