Uchaguzi umeisha sasa kazi Ziendelee, Rais serikali ya Zanzibar

Rais Zanzbar

RAIS wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar dokta ALLI MOHAMMED SHEIN amewataka vijana kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa uchaguzi na kufanya kazi kwa pamoja katika kuijenga upya  jumuiya ya vijana ya CCM.

Dokta SHEIN ametoa rai hiyo leo mjini Dodoma wakati akifunga mkutano mkuu wa tisa wa uchaguzi wa jumuiya hiyo ambapo amesema uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kuelekeza nguvu katika kuijenga jumuiya na chama kwa ujumla.

Mbali na hilo amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kukisemea chama vizuri hasa pale kinaposemwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa upande mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa ndugu KHERI JAMES amewashukuru wajumbe kwa imani kubwa waliyoionyesha kwake na kuahidi kuitumia hotuba ya mwenyekiti wa chama dokta JOHN MAGUFULI kama dira ya kuongoza jumuiya hiyo huku akiwaasa wana UVCCM popote walipo kuzingatia misingi ya chama kwa kupinga na kuwakataa watoa  rushwa.

Aidha amewataka wenyeviti na makatibu wa mikoa kuifanya hotuba ya mwenyekiti wa chama kama ajenda ya kwanza katika vikao ili ijadiliwe katika mabaraza ya mikoa huku akimuagiza kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa SHAKA HAMDU SHAKA kuichapa hotuba hiyo.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments