Ubalozi wa Qatar nchini Tanzania umetoa msaada

img-20161208-wa0004

Ubalozi wa Qatar nchini Tanzania umetoa msaada wa magari kumi ya kubebea wagonjwa (Ambulance)aina ya mercedez benzi, kwa serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya ambapo yamekabidhiwa rasmi hapo jana jijini Dar es salaam kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu

Makabidhiano hayo yamefanyika chini ya balozi wa Qatar nchini Tanzania Bw.Abdalah Bin Jassim Al-Medadi na waziri Mh.Ummy Mwalimu ambapo ameeleza kuwa  yatatumika katika kusaidia wagonjwa mbalimbali katika hospitali za Rufaa na kusaidia kupunguza vifo kwa kinamama na wajawazito na watoto .

Waziri Ummy Amesema kuwa ambulance hizo zitatumika mijini katika hospitali ya  rufaa ya kanda iliyopo Mbeya,mji mwema Kigamboni Gairo,Jakaya Kikwete,Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma na Bombo hospitali iliyopo Tanga.

Ambapo pia jumla ya Ambulance thelasini aina ya Land Cruiser zitatolewa na serikali kupitia wizara ya Afya maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto  kwaajili ya vijijini na mijini ambazo zina uwezo wa kukabiliana na miundo mbinu ya sehemu husika.

#SIBUKA MEDIA LIMITED

Comments

comments