Ubalozi wa marekani jijini Dar es salaam amezindua kituo kipya cha Marekani kilichoanzishwa kwa ubia na maktaba kuu jijini.

Kaimu Balozi kutoka ubalozi wa marekani jijini Dar es salaam DK INMI PETTERSON amezindua kituo kipya cha Marekani kilichoanzishwa kwa ubia na maktaba kuu jijini.

Akizungumza na sibuka fm DK INMI amesema kituo hicho kimelenga kukuza fikra na mijadala ya kina kuhusu masuala mbalimbali kwa kuwapa wananchi haki kupata elimu na taarifa bila vikwazo.

Naye afisa wa maswala ya umma BI BRINILL ELLIS amesema anapongeza sana kwa kuzinduliwa kwa kituo hicho na kusema watahakikisha wanadumisha ushirikiana kati ya marekani na Tanzania ili wananchi wafaidike na program mbalimbali wanazozitoa.

Aidha ameongezea kuwa kituo cha kimarekani kipo wazi muda wote katika maktaba kuu na wananchi wote watakitumia bila malipo na kuwaomba wananchi kutembelea na kujifunza mambo mengi ya kiteknilojia

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments