Tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania {TACAIDS}imesema kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi inatarajia kupungua kutoka 0.32 mwaka 2012 hadi 0.16 ifikapo mwaka 2018.

IMG_3460

Tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania {TACAIDS}imesema kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi inatarajia kupungua kutoka 0.32 mwaka 2012 hadi 0.16 ifikapo mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS ,BW. JUMANNE ISSANGO amesema kuwa maambukizi ya virusi yanaendelea kupungua japo kuna tofauti katika mikoa,wilaya na makundi maalum.

Naye Kaimu Mkurugenzi idara ya muitikio wa kitaifa BI. AUDREY NJELEKELA  ameitaja mikoa inayoongoza kuwa naa maambukizi ya virusi vya ukimwi kuwa ni  NJOMBE,IRINGA,MBEYA na mikoa iliyo chini kwa maambukizi ni MANYARA ,TANGA pamoja na LINDI.

Aidha ameeleza changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na unyanyapaa wanaokutana nao waadhirika wa ugonjwa wa ukimwi ,upungufu wa rasilimali fedha baada ya wafadhili kuondoka pamoja na kuongezeka kwa watoto yatima.

Hata hivyo BW.JUMANNE ameiomba serikali na sekta binafsi pamoja na wananchi kushirikiana katika kutokomeza maambukizi hayo .

  • Mwandishi : Tuse Kasambala.
  • Mhariri : Amina Chekanae
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments