Trump: Tuko nyuma lakini hatukati tamaa.

trump-pence_2016

Maafisa wa kampeni wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Donald Trump wamekiri kwamba mgombea huyo yupo nyuma ya mpinzani wake Hillary Clinton wa chama cha Democratic zikiwa zimesalia chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika.

“Tuko nyuma. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanamfaa yeye (Bi Clinton),” meneja wa kampeni wa Bw Trump, Kellyanne Conway amesema.

Hata hivyo, ameongeza: “Hatukati tamaa. Tunajua kwamba tunaweza kushinda.”

Mnamo Ijumaa, Bw Trump alionekana kukiri uwezekano kwamba anaweza kushindwa.

Alisema iwapo atashinda, ashindwe au atoshane nguvu na mpinzani wake, ataridhishwa na juhudi zake.

Siku moja baadaye, alitangaza hatua ambazo atazichukua siku 100 akiwa uongozini iwapo atashinda.

Miongoni mwa hizo ni kuweka masharti mapya kwenye mchakato wa kisiasa wa kutafuta uungwaji mkono kisiasa, mikataba ya kibiashara na mabadiliko ya tabia nchi.

Kura mpya za maoni zinaonesha Bi Clinton yupo mbele sana kitaifa na katika majimbo mengi yanayoshindaniwa.

Maafisa wake kampeni wa Clinton wamebashiri kwamba huu utakuwa “uchaguzi mkubwa zaidi katika historia ya Marekani”.

Meneja wake wa kampeni Robbie Mook aliambia Fox News Jumapili: “Watu watajitokeza kupiga kura zaidi ya wakati wowote awali.”

Kura za maoni katika majimbo ambayo ni ngome ya chama cha Republican kwa mfano Utah na Arizona zinaonyesha huenda majimbo kwa mara ya kwanza katika miongo mingi akaunga mkono mgombea wa Democratic.

#BBC

Comments

comments