Trump na Clinton kushindania tuzo ya Time

_91356698_trump-clinton

Rais mteule wa Marekani Donald Trump na mpinzani wake wakati wa uchaguzi Hillary Clinton ni miongoni mwa watu wanaoshindania tuzo ya mtu mashuhuri wa mwaka ambayo hutolewa na jarida la Time.

Mshindi atatangazwa Jumatano wiki ijayo.

Kiongozi wa zamani wa chama cha UKIP Nigel Farage, ambaye alitetea Uingereza ijitoe kutoka Umoja wa Ulaya pia ameorodheshwa, sawa na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwenye orodha hiyo ya watu 11.

Wengine ni:

  • Mwanasarakasi wa Marekani Simone Biles aliyefana sana michezo ya Olimpiki
  • Wanasayansi wa CRISPR kutoka Urusi, waliovumbua teknolojia ya kuhariri DNA
  • Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
  • Wakazi wa Flint, Michigan waliofichua kuwepo kwa sumu ya madini ya risasi kwenye maji
  • Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
  • Mwansihili wa Facebook Mark Zuckerberg
  • Mwanamuziki Beyonce

Mshindi wa mwaka jana alikuwa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Comments

comments