Trump matatani ukatili wa kijinsia.

TRUMP

Wanawake walioibua kashafa hiyo dhidi ya Rais Trump ni Jessica Leeds, Samantha Holvey, na Rachel Crooks wamesema kuwa rais Trump bila ridhaa yao alikuwa akiwa shika shika, kuwabusu kwa nguvu na ukatili mwingine. Lakini hata hivyo ikulu ya white house imesema kuwa madai ya wanawake hao si ya kweli

“Rais alikwisha elezea wazi wazi kashfa hizi,katika mikutano yake ya kampeni hata kabla hajawa rais.Na tunaamini kuwa madai haya yalikwisha jibiwa kwa mfumo huo.”Sarah Huckabee Sanders

Rachel Crooks katika madai yake dhidi ya kashfa hiyo ya rais Trump,anasema kuwa yeye alilazimishwa kupigwa busu na rais Trump nje ya lift ya majengo ya ghorofa za Trump enzi hizo akiwa na miaka 22. Japo kuwa mkasa huo ulitokea miaka mingi iliyopita,anasema bado Trumpa anapaswa kuchukuliwa hatua.

  • #SIBUKAMEDIA
  • #BBC SWAHILI

Comments

comments