Trump atangaza vita dhidi ya waandishi.

36339196_303

Mkutano wa waandishi habari wa Donald Trump ulikuwa tangazo la wazi la vita dhidi ya vyombo vya habari vinavyommkosoa, anasema mwandishi mwandishi wa DW mjini Washington Ines Pohl.

Kadiri mammbo yanavyozidi kuvurugika ndivyo inavyozidi kuwa muhimu kurudi hatua nyuma na kutopitwa na yaliyomuhimu. Siku ya Jumatano rais mteule Trump aliitisha mkutano wake wa kwanza na waandishi habari katika nafasi hiyoi. Katika demokrasia, uhuru wa habari ni kitu cha tahamani, kwa sababu wandishi habari ndiyo wawakilishi wa raia katika kuwawajibisha waliopewa dhamana ya uongozi.

Hili linatimizwa kwa upande mmoja kupitia utafiti uliofanywa kwa uangalifu mkubwa, na kwa upande mwingine kupitia maswali magumu kwa mfano wakati wa mikutano ya wandishi habari. mkutano huu ulitangazwa muda mrefu na umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara. Kimsingi mkutano huu ulipaswa kuhusu namna bilinea huyo angehakikisha kuwa hatatumia mamlaka yake ya urais kuzinufaisha biashara zake. Swali hili siyo dogo, kwa sababu linamnufaisha moja kwa moja kwa mfano, wakati wanasiasa na waraghibishi wanapolala katika hoteli zake.

Hata katika biashara zake za kimataifa, wengi wana wasiwasi kwamba rais huyo ajaye atachanganya malengo ya kisiasa na kibinafsi, hata kama siyo moja kwa moja, kwa sababu atakuwa na taarifa kuhusu vitu vinavyoathiri mustakabali wa masoko, hivyo kumpa faida ya wazi dhidi ya washindani wake kibiashara.

#Dw SWAHILI

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments