Trump aisifu Saudi Arabia kwa kuitenga Qatar

DONALD TRUMP

Rais Trump ameungana na nchi ya Saudi Arabia katika mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea na Qatar, huku akiusifu msimamo wa nchi hiyo ya tawala ya kifalme wa kuitenga nchi jirani baada ya Qatar kutuhumiwa kusaidia kifedha makundi yenye msimamo mkali.

Trump ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hatua hiyo inaweza kuwa ndio mwanzo wa kutokomeza tishio la ugaidi. Katika mkutano na waandishi wa habari, msemaji wa ikulu ya Marekani, Sean Spicer, amesema mgogoro huo umekuwa ukifukuta kwa muda mrefu.

“kumekuwa na wasiwasi wa muda miongoni mwa nchi jirani na Qatar. Marekani inaendelea kuwasiliana kwa karibu na nchi zote ili kutatua mgogoro unaoendelea na kurudisha hali ya ushirikiano ambayo ni muhimu kwa usalama wa eneo

  • #SIBUKAMEDIA
  • #BBC SWAHILI

Comments

comments