Timu ya serengeti boys U 17 Afcon 2017 imefanikiwa kuchangiwa zaidi ya milioni 200.

serengeti-boyss11Timu ya serengeti boys U 17 Afcon 2017 imefanikiwa kuchangiwa zaidi ya milioni 200 ili kufanikikisha safari yao kimichezo ambapo tarehe 28 mei mwaka huu watakuwa wakishiriki nchini Gabon.
 
Uchangiaji wa fedha  za kuisaidia timu ya serengeti boys uliongozwa na Waziri mkuu wa nchi mh. Kassim Majaliwa na Waziri wa habari,michezo,utamaduni na wasanii mh.Harrison Mwakyembe pamoja na wadau mbalimbali kutoka asasi zisizo za kiserikali na serikali.
 
Nchi nane zinatarajiwa kuchuana ambazo ni Guinea,Mali,Angola,Mali,Tanzania,Ghanana nyingine ambapo timu mbili zitakazofuzu zitakwenda kushiriki kombe la fainali la dunia litakalofanyika nchini  India.
 
Timu ya serengeti boys U 17 Afcon 2017 imefanikiwa kuchangiwa zaidi ya milioni 200 ili kufanikikisha safari yao kimichezo ambapo tarehe 28 mei mwaka huu watakuwa wakishiriki nchini Gabon.
 
Uchangiaji wa fedha  za kuisaidia timu ya serengeti boys uliongozwa na Waziri mkuu wa nchi mh. Kassim Majaliwa na Waziri wa habari,michezo,utamaduni na wasanii mh.Harrison Mwakyembe pamoja na wadau mbalimbali kutoka asasi zisizo za kiserikali na serikali.
 
Nchi nane zinatarajiwa kuchuana ambazo ni Guinea,Mali,Angola,Mali,Tanzania,Ghanana nyingine ambapo timu mbili zitakazofuzu zitakwenda kushiriki kombe la fainali la dunia litakalofanyika nchini  India.

Akizungumza rais wa TFF Jamal Malinzi amesema kuwa timu ya serengeti boys imekuwa ikicheza katika wakati mgumu na kushukuru bodi ya mfuko wa tff na kueleza bajeti iliyohitajiwa ilikuwa bilioni moja.
Amesema timu ya Serengeti boys imecheza mechi za kimataifa 22 na kushinda mechi 13 na kutoka sare mechi 6.inakabiliwa na michezo minne na inahitaji mechi mbili kushinda ili kuweza kushiriki kombe la dunia.
Nae waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa jitihada za serikali katika kuchangia ni kwakuwa inatambua umuhimu wa michezo na lengo kuu ni kuinua vipaji na ajira kwa vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Nae Waziri wa habari,michezo,utamaduni na wasanii ametoa pongezi kwa wote waliochangia na kusema serikali imejikita katika michezo ili kuwasaidia vijana kupata mabadiliko makubwa na kufikia malengo.
Mwandishi : Tuse Kasambala
#SIBUKAMEDIA

Comments

comments