Tanzania na Afrika Kusini kuanzisha Program ya urithi wa ukombozi.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Jamhuri ya Afrika Kusini zinakusudia kuanzisha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika inayolenga kutunza kumbukumbu zote zinazohusu harakati za Ukombozi wa Bara hilo.

Katibu mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa ELISANTE Ole GABRIEL amewaambia Waandishi wa Habari mjini Dodoma wakati wa Kikao cha maandalizi ya mkutano huo kuwa mkutano wa Mawaziri wa Kisekta kutoka nchi hizo mbili utafanyika siku ya Jumatatu mjini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi rasmi.

Ushiriki wa Tanzania katika harakati za Ukombozi wa nchi nyingi barani Afrika hauna mashaka,kuanzia Mashariki kupakana na Bahari ya Hindi hadi magharibi kwenye fukwe za Bahari ya Atlantiki, kaskazini hadi kusini, kote Tanzania imehamasisha na kukomboa nchi hizo.

Kwa mujibu wa Katibu mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel, malengo ya Programu hii ni kuhimiza Mataifa ya Afrika kutambua, kuhifadhi na kutangaza Urithi wa Ukombozi uliomo katika mipaka yao na kushirikiana kuufanya ujulikane kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments