Tanzania: ATCL kusimamisha wafanyikazi kazi na kuajiri upya

Kampuni ya ndege ya Tanzania ambayo imekumbwa na matatizo kadhaa imepanga kuwasimamisha kazi baadhi ya wafanyikazi wake na kuwa ajiri upya baadhi yao serikali imesema hayo.

Waziri wa Usafiri na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alisema katika Bunge kwamba lengo ni kupunguza namba kubwa ya wafanyikazi katika shirika hilo ambayo iko katika mipango ya mabadiliko.

Aidha anasema Wafanyakazi wote watasimamishwa kazi na baadhi yao wa wataajiriwa upya kulingana na taaluma zao , uzoefu na mahitaji ya shirika la ndege.

Comments

comments