TADB kukopesha wakulima bil 40/-

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) itatumia zaidi ya Sh bilioni 40 kutekeleza mpango wa pili wa maendeleo ya taifa kwa kutoa mikopo kwa vikundi vya wakulima nchini.

Mpango huo wa miaka mitano utaanza kutekelezwa mwaka 2016/17 hadi 2020/21.

Lengu kuu ni kuhakikisha Tanzania inajenga uchumi wa viwanda na kuongeza kiwango cha ajira na uzalishaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Thomas Samkyi alisema haya wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari mjini Dar es Salaam.

benki hiyo imeamua kusaidia utekelezaji huo ili kuwezesha upatikanaji wa usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini.

mikopo hiyo inalenga kuwanufaisha wakulima wadogo, wa kati na wakubwa kwa ajili ya kuziba pengo la upatikanaji wa fedha katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi.

Aidha bw; Thomas anasema benki hiyo tangu kuanzishwa kwake imetoa elimu kwa wakulima na kuwawezesha kupata mikopo.

Comments

comments