Taasisi ya watetezi wa haki za binadamu tanzania (THRDC) umeandaa warsha kwa asasi za kiraia nchini .

sungusia
Taasisi ya watetezi wa haki za binadamu tanzania (THRDC) umeandaa warsha kwa asasi za kiraia nchini jinsi ya kufatilia matukio ya mateso yaliokwisha ripotiwa katika vyombo husika na kuhakikisha yanchukuliwa hatua stahiki. 
Akizungumza ktk ufunguzi wa warsha hiyo wakili wa kujitegemea bw Havold Sungusia alisema lenfo la warsha hii ni kuhamasisha wawakilishi wa mashirika ya asasi za kiraia kukemea matendo yanayotokea kama mateso pamoja na kuzijengea uwezo asasi hizohili ziweze kukemea vitendo hivyo vya unyanyasaji sambamba na kushawishi tanzania kuridhia mkataba wa umoja wa mataifa dhidi ya mateso (UN CAT). 
Alisema warsha hiyo pia itajikita zaidi ktk kuongeza ufahamu kwa asasi hizo juu ya namna ya kukemea matukio ya mateso yanayojitokeza katika jamii zetu na namna ambavyo wanaweza kufatlia matukio hayo ili kuyapatia ufumbuzi. 
Aidha bw sungusia aliongeza kuwa lengo la mtandao huo ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kukemea mateso ili kuweza kujikita zaidi kama nchi kuheshimu ibara ya 5 ya tamko la haki za binadamu la mwaka 1948 sambamba na ibara ya 7 ya mkataba wa kimataifa wa haki za kisiasa na kiraia ya mwaka 1966.
Alisema matukio ya mateso ni swala mtambuka katika maswala mbalimbali hivyo taasisi hiyo imeona hipo haja kuanzishwa kwa mtandao wa pamoja wa asasi za kiraiakupinga uteswaji na unyanyasaji kinyume na haki za binadamu.
Imeandaliwa na Tuse Kasambala.
#SIBUKAMEDIA

Comments

comments