Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo AMDT yenye makao makuu yake jijini Arusha imezindua mradi wake mkoani Singida ikiwa na lengo la kukuza na kuendeleza kipato kwa wakulima hususani wa Alizeti.

SINGIDA
Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo AMDT yenye makao makuu yake jijini Arusha imezindua mradi wake mkoani Singida ikiwa na lengo la  kukuza na kuendeleza kipato kwa wakulima hususani wa Alizeti.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya SINGIDA,katibu tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoa wa SINGIDA, STANSILAUSI CHOAJI amelishukuru shirika hilo kwani ni fursa kwa mkoa wa Singida kuendeleza na kukuza zao la alizeti ambalo ndio zao kuu la biashara ndani ya mkoa wa singida.

Akisoma Risala mbele ya mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Faida mali mkoani SINGIDA BW.TOM SILAYO amesema wamekuwa wakitoa mafunzo katika makundi mbalimbali ya wakulima ikiwemo kilimo biashara.

Nae Mwenyekiti wa ushirika wa wakulima wa alizeti Tanzania BW.PETER HELLY amesema mradi wa AMDT utasaidia kutatua changamoto za wakulima wa zao hilo ndani ya mkoa huo.

Kwa upande wake BI. CATHERINE KIONGO ambae ni mmoja wa wakulima wa zao hilo la Alizeti  ameshiriki uzinduzi huo na kusema kushuka kwa bei ya Alizeti sokoni ndiyo Changamoto kubwa wanayokumbana nayo wakulima wa zao la alizeti.

 

# imeandaliwa na SAULO STEVEN

# Imehaririwa na Amina Chekanae

 

Comments

comments