Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa kilimo cha kitropiki (IITA) leo imeadhimisha siku ya umuhimu wa mimea duniani.

Bw.Victor Manyong.

Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa kilimo cha kitropiki (IITA) leo imeadhimisha siku ya umuhimu wa mimea duniani kwa kusherehekea na watoto wa shule ili waweze kujifunza masomo ya kisayansi kwa  bidii.

Akizungumza katika maadhimisho hayo mkurugenzi mtendaji taasisi ya kimataifa ya utafiti wa ya kilimo cha kitropika (IITA),  Bw.Victor Manyong alisema taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha  na utafiti wa kilimo ili kuwasaidia wakulima katika mchakato wa kilimo na ndiyo mana siku hii hushirikisha watoto ambao ni vema wakipata mafunzo tangu awali ili kufikia mafanikio ya kisayansi.

Mkurugenzi Manyong amesema kuwa changamoto mbalimbali zimekuwa zikiwakabili wakulima kwa kukosa vitendea kazi vya kisasa pamoja na upungufu wa pembejeo na mbegu.

Bi Catherine Njuguna.

kwa upande wake afisa mawasiliano wa Taasisi hiyo Bi Catherine Njuguna alisema matokeo ya tafiti zao ambazo wamekuwa wakifanya sehemu mbalimbali nchini wamegundua kuwepo na changamoto nyingi sana hususani magonjwa ya mimea.

Amesema pamoja na wataalamu kushauri juu ya njia bora za kutumia kwa wakulima hususani wadogo bado kumekuwepo na mwamko mdogo kwao hususani katika swala la matumizi sahihi ya pembejeo pamoja na ushauri wa wataalam wa kilimo.

Maadhimisho ya siku ya umuhimu wa mimea duniani huadhimishwa tarehe 14 mwezi mei.

  • Mwandishi : Tuse Kasambala.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments