Taarifa za kodi za Donald Trump za mwaka 2005 zafichuliwa.

Bw Trump alikataa kufichua taarifa zake za malipo ya kodi .
Bw Trump alikataa kufichua taarifa zake za malipo ya kodi .

Rais wa Marekani Donald Trump alilipa kodi ya jumla ya $38m (£31m) kwa mapato yake ya $150m (£123m) mwaka 2005, taarifa za malipo yake ya kodi ambazo zimefichuliwa zinaonesha.

Taarifa ya kurasa mbili ya malipo yake ya kodi ilifichuliwa na runinga ya MSNBC ya Marekani, jambo ambalo limekera sana ikulu ya White House.

Maafisa wa ikulu wamesema ni kinyume cha sheria kuchapisha taarifa hizo.

Bw Trump alikataa kutoa taarifa zake za malipo ya kodi wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais, hatua iliyoenda kinyume na utamaduni wa wagombea urais nchini Marekani.

#SIBUKAMEDIA

#BBC SWAHILI

Comments

comments

Random Posts