SUMAYE ASEMA KUKOSEKANA KWA DEMOKRASIA BARANI AFRIKA KUNACHANGIA NCHI NYINGI KUWA MASIKIN

lll

DAR ES SALAAM

Imeelezwa kuwa kukosekana kwa demokrasia na utawala bora barani AFRIKA kunachangia nchini nyingi barani humu kuendelea kuwa maskini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kanda ya PWANI,FREDRICK SUMAYE wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM.

Amesema ili kuondokana na hali hiyo nchi za AFRIKA zinapaswa kuangalia kwa makini mfumo wa utawala uliopo katika nchi nyingi barani AFRIKA.

Akizungumzia mgogoro uliopo ndani ya Chama cha Wananchi(CUF)na madai ya CHADEMA kuhusika na mgogoro huo SUMAYE amesisitiza kuwa CHADEMA hawahusiki na mgogoro huo na kwamba mgogoro huo unachochewa na chama tawala.

Mwandishi:Tuse Kasambala

Comments

comments