Stanislav Petrov, aliyezuia vita vya nyuklia wakati wa Vita Baridi afariki akiwa na miaka 77.

ZZZ

Afisa wa zamani wa jeshi la Muungano wa Usovieti ambaye anasifiwa sana kwa hatua yake ambayo huenda ilizuia vita vya nyuklia kati ya Marekani na muungano huo wakati wa Vita Baridi amefariki dunia akiwa na miaka 77.

Stanislav Petrov alikuwa kwenye zamu katika kituo cha Urusi cha kutoa tahadhari kuhusu nyuklia mapema siku moja mwaka 1983 mitambo ya kompyuta ilipofanya makosa na kutoa tahadhari kwamba kulikuwa na makombora yaliyokuwa yamerushwa na Marekani kuelekea Urusi.

Alichukua uamuzi wa busara kuamua kwamba tahadhari hiyo haikuwa sahihi.

Aidha, hakupiga ripoti kwa wakuu wake.

Kitendo hicho chake, ambacho kilifichuliwa baadaye, huenda kilizuia vita vya nyuklia.

  • #BBC SWAHILI
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments